Epuka Giza kaa Nuruni HD 1080p
1Yohana 1:5-10
Ujumbe ndiyo huo 5a
Mungu ni Nuru hana Giza 5b
Watu wa giza 6
Watu wa Nuru 7
Kudai hatuna dhambi n ikujidanganya 8
Dhambi inatakiwa kushughulikiwa 9
Kusema hatutendi dhambi ni kumfanya Mungu mwongo 10
1Yohana 1:5-10
Mungu ni nuru
5 Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lolote hamna ndani yake. 6 Tukisema ya kwamba tunashirikiana naye, huku tukienenda katika giza, tunasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli; 7 bali tukienenda katika nuru, kama yeye alivyo katika nuru, tunashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. 8Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe, wala kweli haimo ndani yetu. 9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kututakasa na udhalimu wote. 10Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, tunamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo ndani yetu.
Ujumbe ndiyo huo 5a;
Yohana anarudia tena kusema kwamba ujumbe anaouleta ni yale aliyoisikia kwa Yesu mwenyewe.
Si ujumbe aliyobuni mwenyewe bali ni maneno ya Mungu.
Mungu ni Nuru hana Giza 5b
Nuru inalinganishwa na kinyume cake Giza
Nuru na Giza havina ushirikiano, mmoja akiingia mwingine lazima ataondoka.
Yesu anajitangaza kama ”Nuru ya ulimwengu” Yoh 8:12
Mfano wa Mungu kama nuru ya watu wake tunaiona katika Kutoka 13:21
Baadhi ya maandiko yanayoongea juu ya Mungu kuwa nuri;
Mungu ni Nuru yetu
Zab 27:1, 119:130
Yesu ndiyo hiyo nuru kwa vile naye ni Mungu
Yoh 1:4; 8:12; 9:5; 11:9-10; 12:35-36
Maana yake Mungu;
Ha danganyi - Habadiliki - Kauli yake ni kweli - Hana dhambi - Yuko wazi katika habari zake zote.
Watu wa Giza 6
Kuna watu wanaodai kuwa wamo katika Nuru, lakini mambo yao yanawa saliti!
Mtu asiye tembea Nuruni na kuruhusu ukweli wa Mungu kummulikia si mtu wa Nuru bali wa Giza, ni mwongo na hana ushirikiano na Mungu.
Ukiendelea na dhambi katika maisha, hauko na Mungu, usijidanganye!
Watu wa giza Yohana anasema juu yao katika Yohana 3:19-21
Watu wa Nuru 7
Kama vile ilivyo na watu wa Giza hata watu wa Nuru wanatambulika,
Wanaushirikiano na watu wa Mungu wengine
1Yohana 5:1 inasema;
alama nynigine ni kwamba wanajiepusha na dhambi, wanapotambua dhambi maishani wanaiungama na kuliacha.
Hawatetei dhambi kama ”matatizo kidogo”, ”kila mtu anafanya…” bali wanashughulikia!
Kudai hatuna dhambi ni kujidanganya 8
Anaye sema hana dhambi, anajitambulisha kama asiye tembea katika nuru!
Biblia inasema kwamba sote tumeambukizwa dhambi kwa urithi kutoka adamu na Hawa Warumi 5:12;
Katika Waebrania tunasoma; 4:12-13
Haina maana kujidanganya, ipo siku ya mahesabu bora kuanza kushughulikia dahmbi leo!
Dhambi inatakiwa kushughulikiwa 9
Mungu si Mungu wa kutuweka katika hali isiyo na uponyaji
Anasema hivi katika andiko lake mst 9
Hatuachi bila njia!
Tunahitaji kukiri kila dhambi maishani mwetu
Mawazo - Matendo - Tabia - Maneno …
Tunapokiri Yeye naye ni;
MWAMINIFU na wa HAKI
ANAONDOA DHAMBI ZETU
ANANTUTAKASA NA UDHALIMU WOTE!
Kusema hatutendi dhambi ni kufanya Mungu kuwa mwongo 10
Licha ya hali ya dhambi tuliyonayo, tunaungama tunapomwendea Mungu na kutubu
Tunaendelea kutenda dhambi kila siku, kwa hiyo tunahitaji kukaa katika ungamo kila siku…
Utakaso ni jambo la maisha yote, tunapozidi kutakaswa dhambi ndogo zonzjitokeza, na tunayashughulikia.