Up next

SIKU YA TATU | NOVENA YA ROHO MTAKATIFU | TUNAOMBA KUPATA UTAKATIFU

4 Views· 06 August 2023
proshabo
proshabo
5 Subscribers
5

NOVENA YA ROHO MTAKATIFU
SIKU YA TATU
TUNAOMBA KUPATA UTAKATIFU
Ewe Roho Mtakatifu, chanzo na undani wa maisha yetu na unayetutakatifuza, ninaomba bila kuchoka unisaidie kufungua akili yangu ielekee kwenye ukweli. Uuguse moyo wangu na uweze kunitakatifuza, na kuulinda moyo wangu kama ulivyoulinda Moyo wa Mama yetu Maria na mashaidi na Watakatifu wote. Ninayo nia na hamu kubwa ya kupata utakatifu, sio kwaajili yangu bali kwaajili ya utukufu wako wewe Bwana wa mabwana, utukufu katika utatu, usitawi wa kanisa na mfano bora kwa wale waliotangulia kufika kwako. Hakuna njia iliyo nzuri zaidi ya kuwa mitume kweli pasipo kuwa Mtakatifu, kwani bila utakatifu tunaweza kukamilisha kazi kidogo sana. Roho Mtakatifu sikiliza sala yangu na uitimize hamu ya moyo wangu.
Tuombe:
Ewe Roho Mtakatifu, nafsi ya moyo wangu vinakuabudu, niongoze kwa mwanga wako, nipe nguvu, nifariji, nifundishe nipaswayo kufanya, na unipe sheria yako. Naahidi kuyatoa maisha yangu kwaajili ya kutekeleza mpango wako. Mimi ninaomba tu kufahamu matakwa yako.

Show more

 0 Comments sort   Sort By


Up next