Up next

TAFAKARI YA KWARESMA: SIKU YA 5 - ONA UCHUNGU JUU YA DHAMBI ZAKO NA PADRE PROSPER KESSY

2 Views· 01 September 2023
proshabo
proshabo
5 Subscribers
5

Sasa sisi tujue kwamba kama dhambi zetu zingekuwa zinafuatiliwa kama za mwenzangu au za yule ninayemsema-hakika ningalikuwa gerezani tayari. Nakueleza-waliopo gerezani sio kwamba ndio wenye dhambi sana. Wapo kati yetu kama makosa yetu yote yangalikuwa yamejulikana-nakueleza ungalikuwa jela tayari. Hivyo, jua hili kwamba wapo ambao dhambi zao zinatangazwa zaidi ya wengine na ndio maana wanakuwa victims. Kwa mfano-padre dhambi zake hutangazwa kuliko za mtu wa kawaida.
Ukiona wale mafisadi wanaburutwa gerezani-usicheke-ni kwa sababu wao wanafuatiliwa, vyombo vya habari vinawamulika kila mahali. Na wapo wengine wanauziwa hata kesi. Hili ulijue ili upate kufanya toba ya ndani.
Hizi ni tabia zinazotuua kiroho, kamwe usijilinganishe na mwanadamu. Utaishia kuwa mwizi. Umeelezwa kwamba tuwe wakamilifu kama baba yetu alivyomkamilifu. Hivyo, tuachane na kujilinganisha na mwanadamu mwenzetu ndugu yangu.
Huyu mtoza ushuru alikuwa hajagi hekaluni mara kwa mara na hivyo hata alipokuja, ilikuwa ndio mara ya kwanza ya kwanza kwanza kukutwa pale. Alikuwa hakutwagi mara kwa mara. Naye anapaswa ajiongeze japokuwa Yesu kamsifia leo. Ajiongeze, aache uvivu, aache uvivu. Sio ati kwa kujisikitia dhambi zake ndio aishie hapo, anapaswa kupanda juu zaidi, juu sana. Abadilike, awe mtu mwema. Na wewe fanya hivi.

Sasa, pale unapoingia hata kama ni kanisani na kumkuta ambaye ni mdhambi zaidi yako-isikufanye uanze kujifikiria ati kwamba upo vizuri-ukimkuta akufanye wewe ukazane, ujione kwa hakika kwamba wewe ni mvivu, uwepo wake ukufanye wewe ujiongeze pia na sio kujisifia sifia na kujisahau kabisa. Nyanyuka kama vile na mtoza ushuru anavyopaswa kunyanyuka.
Niendelee kwa kuongelea tena kuhusu kipindi hiki cha ugonjwa wa korona. Hii kutokuhuzunikia dhambi ni mbaya zaidi kuliko korona. Ukiangaliaa kila mahali tunaogopa korona, yaani tumechukua tahadhari ajabu, hata watu hawaji tena mjini kuzunguka. Watu wanaogopa hata kukushika mkono, watu wanoogopa hata kukomunika-yaani tumekuwa na hofu ajabu. Hata mimi ninayo hofu kubwa sana ninapoongea nanyi na kuna wakati naonyesha hofu hata kushika mkono wa mtu au hata kumkomunisha mtu mdomoni. Naogopa nisigusane na mate yake. Ni kweli lazima nichukue tahadhari na tunamwomba Mungu atuondeshee huu ugonjwa. Kakini tutambue kwamba dhambi zetu ndio korona ya juu kabisa na mbaya kuliko zote.
Korona unaweza kukaa nayo kwa muda wa siku 14 bila ya chochote kuonekana na kumbe unawaambukizia wengine. Ndivyo na kutokuhuzunikia dhambi zetu. Tunaweza kuishi na dhambi zetu, tukikaa na marafiki wazuri, hata tukawa rafiki kwa mapadre-lakini mwisho wa siku dhambi hizi zitabakia kuwa zetu na hivyo zitakuja kutuadhibu kama Corona inavyokujaga kuadhibu mbeleni baada ya kukaa nao kama rafiki. Hivyo, epuka urafiki na dhambi zako kama unavyopaswa kuepuka urafiki na virusi vya korona. Vinajidai vinakupenda lakini mwishowe vinakuja kuwa adui. Na wewe tabua hilo ndugu yangu.
Kama Korona inavyoendelea kuambukizwa kwa wengi wakati bado vikiwa vimejificha, ndivyo ilivyo hatari au maumivu yaletwayo na kutokuhuzunikia dhambi inavyosababisha madhara. Wewe ukijiona na afya-na kumbe ukaendelea kuwasambazia wenzako dhambi na kuwafundisha ubaya, hakika unakuwa kama vizuri hivi vya korona. Navyo vina jitabia kama hizi. Vinajificha na kumbe vinasababisha madhara makubwa.
Virusi vya Korona hufanya kifua chako kibane na kushindwa kupumua. Ndivyo kutokuhuzunikia dhambi zinavyotukaba na kushindwa kupumua na kushindwa kuongea mbele za watu. Hivyo, korona ni ndogo zaidi kuliko kutokuhuzunikia dhambi zetu.
Virusi vya Korona vimetufanya tuongope hata kuwashika wengine mkono, hata kupakia daladala, hata nipumue hewa ya kawaida. Lakini kutokuhuzunikia dhambi ndiyo inayotufanya tushindwe kuwashika wenzetu kuwapatia mkono wa heri, itatufanya tushindwe kufanya mkusanyiko wowote na kufanya canceling kama wengi tunavyofanya canceling ya booking za ndege. Tutafika kanisani bila kujuana, ukimtakia mwenzako amani wala moyo wako haupo hapo, hivyo tuwe watu wa kuhuzunikia dhambi zetu ndugu zangu.
Corona imetufanya tuoogope tufunge makanisa-lakini hii kutokuhuzunikia dhambi zetu ndizo zilikuwa chanzo-na ni sababu ya hata makanisa yetu yafungwe sasa na baadaye-corona itafunga kanisa kwa sasa lakini dhambi itaufnga kwa nyakati zote
na wapo wanaofurahia ati makanisa yanafungwa kwa sababu ya Corrona wakisema ati Mungu sasa hana nguvu. Lakini ukitafakari wewe huna tofauti na hawa wanaofurahi-sisi tusiohuzunikia dhambi zao. Ndio tunapofurahia tukiona ati mwingine kaanguka-ni sawasawa na huyu anayeona kanisa limefungwa-watu hawawezi kusali tena na hivyo kuamua kufurahia.sisi tuipinge dhambi kuliko korona
Korona inatutuka tufuate masharti-kuwa na sanitizer na maji ya kunawa sasa ni kila mahali. Sasa nasi tuwe na maji ya kusafisha dhambi zetu. Ni sakramenti ya kitubio. Kama tulivyoserious kwenye kunawa mikono kwa sababu ya korona tufanye hivyo hivyo kwenye dhambi zetu.

#jugomedia #kanisakatoliki #familiatakatifu #wawata #uwaka #viwawa

Show more

 0 Comments sort   Sort By


Up next