Up next

3. DALILI ZA KURUDI KWA YESU NA UNYAKUO WA KANISA | Mwl. Isaac Javan

5 Views· 14 August 2023
proshabo
proshabo
5 Subscribers
5
In Sermons

Tunakaribia mwisho wa dunia hii, na YESU yupo karibu kuja kulichukua kanisa lake. Kama Mungu amekupa nafasi ya kuwa hai siku ya leo, fahamu ya kwamba unaishi kwenye kipindi muhimu sana kwenye historia ya maisha ya mwanadamu.

Mambo tunayoyashuhudia leo, ni mambo ambayo manabii waliopita walitamani kuyaona lakini hawakuyaona. Mambo tunayosikia, ni mambo ambayo manabii walitamani kuyasikia, lakini hawakuyasikia. Sisi tumepewa kibali na neema ya kuishi na kushuhudia unabii ukitimia mbele ya macho yetu.

Hili somo linakuja kwako ili kukuandaa kunyakuliwa, kwa sababu YESU yupo karibu sana kurudi. Hakikisha unasikiliza vizuri mafundisho haya, halafu uweke kwenye matendo kile utakachojifunza, ili parapanda ikilia, na wewe uwe mmoja wa tutakaomlaki YESU pale mawinguni.

Nakuombea YESU akutie nguvu ya kusimama katika imani yako ndani ya KRISTO. Nakuombea utunze vazi lako la wokovu, ili shetani asije akaitwaa taji yako. Nakuombea tumaini lenye baraka la kunyakuliwa lisikupotee, lakini ukae tayari kwa sababu saa yaja, nayo sasa ipo. YESU anarudi.

Mungu akubariki. Mshirikishe na ndugu, jamaa na marafiki zako juu ya ujumbe huu muhimu. Amani ya YESU iwe ndani yako. Amen

Mwl. Isaac Javan

Show more

 0 Comments sort   Sort By


Up next