Bella Kombo Ft solomon mkubwa-Mkono wako (official video)
wimbo umeandikwa na Bella Kombo akishirikiana na Solomon Mkubwa.
Audio production: Gamba Production
Video production: Solomon K
LYRICS
Mahali nimefika nimeuona mkono wako
Mahali ninapokwenda utaniongoza Bwanaa
Mahali nimefika nimeuona mkono wako
Mahali ninapokwenda utaniongoza Bwana
chorus
Mahali nimefika imegharimu mkono wako
Mahali niendapo tena utaniongoza Bwana
verse 1
Kwenye hii safari ya Mbingu nahitaji kushikiliwa nawe
Bila wewe Bwana siendi mahali mzee wangu wa siku nakuhitaji Bwana
Nishike mkono Bwana wangu vitisho ni vikali saana
Bila wewe sitaweza vuka niongoze nivuke ng'ambo
chorus
Mahali nimefika imegharimu mkono wako
Mahali niendapo tena utaniongoza Bwana
verse 2
Asiuache mguu usogezwe asisinzie yeye hatalala
Wenye kiburi wamenidharau sikujiepusha na sheria yako unifundishe
Maana msalaba ndiyo asili yangu Msalaba ndio kiburi mbele ya adui
Unifundishe nami nitasikia usiuache mguu wangu eeeh Baba
chorus
Mahali nimefika imegharimu mkono wako
Mahali niendapo tena utaniongoza Bwana
bridge
Umekuwa jiwe langu umekuwa jabali langu
Umekuwa ngome yangu utaniongoza Bwana
Utaniongoza Bwana
Utaniongoza Bwana......