Bwana Uliyewaita (Nyimbo za Tenzi nambari 67)
0
0
4 Views·
01 September 2023
In
Gospel Songs
Bwana uliyewaita
Watakatifu wako
Wawe mitume, wachunga
Walishe kundi lako
Wanyonge na wenye hofu
Wakawa mashujaa
Na wapole wa kunena
Wasiwe kunyamaa
Hata leo wawataka
Watakatifu wako
Nawe wauliza tena
Ni nani aliyeko
Atakaye nimtume
Afundishe vijana
"Ni tayari Bwana wangu
Nitume mimi Bwana
Nitume na mimi Bwana
Kama ulivyotumwa
Habari ya msamaha
Na dhambi kutubiwa
Niwahubiri wakosa
Na waliopotea
Wokovu ni wake Bwana
Aliyewafilia.
Astahiliye hapana
Kutamka habari
Lakini wewe waweza
Kutufanya tayari
Neno Lako tulijue
Tupe na Roho wako
Hayatakuwa ya bure
Haya Maneno yako
Show more
0 Comments
sort Sort By