Cha Kutumaini Sina | Sauti Tamu Melodies | kwaresma | Nyimbo za Sifa (sms SKIZA 5814855 to 811)
Cha kutumaini sina, ila damu yake Yesu, sina wema wa kutosha, dhambi zangu kuziosha
Kwake Yesu nasimama, ndiye mwamba ni salama, ndiye mwamba ni salama, ndiye mwambani salama
Njia yangu iwe ndefu yeye hupia wokovu, mawimbi yakinipiga, nguvu zake ndizo nanga
Damu yake na sadaka nategemea daima yote chini yakiisha, Mwokozi atanitosha
Nikiitwa hukumuni, rohoni nina amani, nikivikwa taji yake, sina hofu mbele zake
#SautiTamu #tenzizarohoni #kwayakatoliki
Wimbo: chakutumaini sina
Mtayarishaji - Martin Mutua Munywoki
Kinanda - Martin Munywoki
Waimbaji - Sauti Tamu
Extra clips from Cheers and Tears movie by Munywoki M. M
chakutumaini sina ni wimbo wa kuabudu, unaweza tumika pia kama wimbo wa huzuni, wimbo wa mazishi, matanga, maombolezo, nyimbo za msiba n k
wakati mwingine unatumika wakati wa kupokea mwili na damu ya Yesu.
Tazama nyimbo nyingine za sifa na kuabudu kwa channel hii kama vile huniongoza Mwokozi, chakutumaini sina, atukuzwe aleluya, roho yangu na ikuimbie, na Lo Ajabu kupata uzima.
unaweza tumika kipindi cha Kwaresma, lent