Up next

EPUKA KUJIHURUMIA (Be willing to avoid excuses)- Askofu Amon Lukama

3 Views· 01 September 2023
proshabo
proshabo
5 Subscribers
5

Katika maisha lazima uwe tayari kuepuka kujihurumia na kua na vijisababu.
Mambo yatakayo changia kufeli kwako.
1. Kukosa maono
- Maono yanajibu swali la nini ufanye
- Na malengo yataleta namna ya kufanya
2. Kukosa maarifa
- Maarifa yanaweza kutafutwa na kupatikana
- Na ni ya muhimu sana
3. Kukosa utii
- Utii ni muhimu sana katika maisha
4. Kuwashusha walio fanikiwa/ Kutoa sababu kwanini wengine wamefanikiwa/ kukosoa mafanikio ya wengine.
- Ili ufanikiwe jifunze kwa wale walio fanikiwa

Lazima uondokane na vijisababusababu
Hesabu 13: 1-2, 21-24, 27-29, 33
1-2
1 Kisha Bwana akanena na Musa, akamwambia,
2 Tuma watu, ili waende wakaipeleleze nchi ya Kanaani, niwapayo wana wa Israeli; katika kabila ya baba zao mtamtuma mtu mmoja, kila mtu na awe mkuu kati yao.

21-24
21 Basi wakapanda wakaipeleleza nchi toka jangwa la Sini hata Rehobu, mpaka kuingia Hamathi.
22 Wakapanda katika Negebu, wakafika Hebroni; na Ahimani, na Sheshai, na Talmai, wana wa Anaki, walikuwako huko. Nao Hebroni ulijengwa miaka saba kabla ya Soani wa Misri.
23 Wakafika bonde la Eshkoli, na huko wakakata tawi lenye kishada kimoja cha zabibu, wakalichukua kwa mti kati ya watu wawili; wakaleta makomamanga pia, na tini.
24 Bonde lile liliitwa bonde la Eshkoli kwa sababu ya hicho kishada walichokata huko wana wa Israeli.

27-29
27 Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake.
28 Lakini watu wanaokaa katika nchi ile ni hodari, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa sana; na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko.
29 Amaleki anakaa katika nchi ya Negebu; na Mhiti, na Myebusi, na Mwamori wanakaa katika milima, na Mkanaani anakaa karibu na bahari; na kando ya ukingo wa Yordani.

33
33 Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.

Mtazamo hasi ni mbaya, utakufanya ujione si kitu
- Maendeleo ya mtazamo chanya ni muhimu sana katika kufanikiwa kwako,
- namna unaona vitu ni muhimu, na inajalisha sana.
- Mungu anapokuita, atakutia nguvu kwa ajili ya kazi aliokuitia. Maana hio kazi itaendana sawasawa na neema Mungu alioachilia kwako.

mithali 26:13
mtu mvivu husema simba yupo njiani, simba yupo njia kuu.

Ungana na Askofu Amon Lukama katika kutafakari neon kila alhamisi.

Mawasiliamo 0764982929

Show more

 0 Comments sort   Sort By


Up next