Fid Q - Tajiri Yangu Feat Paul Clement (Official Video)
#FidQ #TajiriYangu #PaulClement #SlideDigital
All praises due to the most high..
TAJIRI YANGU LYRICS:
Verse 1: ( Fid Q )
Lord.. ni ngumu kujua wewe uko wapi ila unajua nilipo/ ninaisaka haki kuipata ni bahati na kwa waganga siko/
Vyuma vikikaza tunatangatanga kuuchanga mshiko.. na mbanga zinakwaza madada wakidanga wanabamba vifo/
Na waliopinda wewe huwalinda na love/
Ka wale wajinga ambao hunipinga ninapouwinda wokovu/
Haunipi shida bila namna ya kuisolve/ wewe ndio mmiliki wa kila tiba na hauna iliyo mbovu /
Hauna iliyombovu.. unanipa uinchaji na power.. unaninyanyua juu/
Ni zaidi ya dawa.. sikuhitaji ninapougua tu/
Unaniweka sawa.. devil akitua hamchukui Q/
Una uwezo wa kunigawa au kuniumbua.. sio tu kuniumba mkuu/
ni rhumba tu ndio linaweka vumba juu na nakututesa kama mfungwa anayechungwa nakudundwa juu/
Wewe ndio BOSS ninayekuamini.. haututosi tukichomewa/ sio wale wanaowahi kazini ili wafoke tukichelewa...
Chorus ( Paul Clement )
Ewe Ewe.. tajiri yangu/
Wewe ndiwe kila kitu kwangu/
Ewe Ewe tajiri yangu/
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
Ewe tajiri.. wa matajiri..
Ewe tajiri..Tajiri yangu/
Verse 2: ( Fid Q )
Mwanadamu amemtawala mwanadamu kwa kumuumiza/
Anakwapua mpaka asivyovihitaji bila kubakiza/
Hii inafanya nafsi yangu ikose subira/
Ikose usingizi, uoga., huzuni na hasira/
kwangu furaha ni kuwa na Mungu sio mlungura/
Na pia siku zote mla raha na uchungu hula/
Ninajua nilipotoka na ninajua wapi nilipo/ ispokuwa ni wewe pekee unajua lini nitafika mwisho/
cheo chako ni kirefu zaidi ya dunia... kipana zaidi ya bahari.. ulinzi mkali hakuna Askari anayefikia/
Ninamlaani shetani kiundani nipate kukujua mkuu/ ili nijihami na mtihani nisiache tusua Q/
Ninajua una huruma naomba nikibuma usinitose/ mwanadamu atazingua.. heshima sio utumwa kwa boss/ hawezi nunua uhai.. anajidai kwa lipi?/ na kwako sio tu akeshaye hata alalaye humpa riziki..
Chorus ( Paul Clement )
Ewe Ewe.. tajiri yangu/
Wewe ndiwe kila kitu kwangu/
Ewe Ewe tajiri yangu/
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
Ewe tajiri.. wa matajiri..
Ewe tajiri..Tajiri yangu
Bridge ( Paul Clement )
Siwezi kuwa masikini sababu../
Anayenitunza ni tajiri.. ni Mungu/
Asiyeacha nigange njaa, nikosee furaha.. nikate tamaa/ eeh wee eeh wee tajiri yangu
Chorus ( Paul Clement )
Ewe Ewe.. tajiri yangu/
Wewe ndiwe kila kitu kwangu/
Ewe Ewe tajiri yangu/
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
Ewe tajiri.. wa matajiri..
Ewe tajiri..Tajiri yangu
FID Q Songs OUT WORLDWIDE ON MAJOR DIGITAL STORES:
Written & Performed by Fid Q
Follow Fid Q on:
https://www.instagram.com/therealfidq/
https://twitter.com/FidQ
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz