Up next

Jinsi ya kusikiliza Roho Takatifu | Clairaudience | Nguvu za miujiza l Kusikia zaidi ya kawaida

1 Views· 10 August 2023
proshabo
proshabo
5 Subscribers
5

Katika video hii nitazungumzia nguvu nyingine ya muujiza moja kati ya nguvu za miujiza walizonazo watu wengi ambayo ni Clairvoyance;

UWEZO WA KUSIKIA ROHO TAKATIFU CLAIRAUDIENCE l NGUVU ZA MIUJIZA

Hii ni moja kati ya nguvu za miujiza ambayo wenye nayo huitwa clairvoyants hawa hutambulika kama watu wenye uwezo wa kuona yajayo;

Chochote kinachohusu jambao linalokuja kama vile kwa mtu,kitu au eneo.

Wenye uwezo huu wengine huwaita walii yaani vipenzi vya mwenyezi Mungu.

Hapa nitakuelezea juu ya nguvu ya miujiza walionayo watu hawa huenda wewe pia unayo lakini hujifahamu.

Clairvoyance ni uwezo ambao mtu huwa nao ambao humsababisha kuweza kuona yanayokuja mbele yaani fikra au maono yake yana kuwa na uwezo wa kuona yajayo (future).

unachotakiwa kuelewa kwanza neno hili ‘clairvoyance’ limetokana na lugha ya kifaransa kwa maana ya utengano wa maneno mawili yaliyoungana yaani clair na voyance ikiwa na maana kwamba neno ‘clair,’ ni clear kwa lugha ya kingereza ambapo kiswahili tunasema ni wazi hivyo kivumishi chake kinakuwa ni -eupe na kitenzi chake ni safi au safisha,

kwa wataalamu wa kiswahili watakuwa wanafahamu naongelea nini na voyance ni vision kwa kingereza ambayo kwa kiswahili ni maono.

hivyo basi;

kwa maana nyepesi ni kwamba Clairvoyance ni maono ya wazi au maono meupe yasio na doa au shaka ingawa imegawanyika katika vipengele tofauti tofauti vya kuweza kuona yajayo sasa kuna matawi ya Clairvoyance lakini hapa tutaanza na clairaudience;




ambapo;

Clairaudience;

maana yake ni kusikia kwa uwazi yaani nguvu ya miujiza yenye kumuwezesha mtu kuweza kusikia sauti kutoka kwenye ulimwengu wa roho kama vile wanyama wanavyoweza kusikia sauti za watu makaburi basi kuna wanadamu pia wamejaliwa uwezo huo.


Clairaudience ni nguvu ya kiroho ambayo humsaidia mtu katika kuwa na uwezo wa kusikia sauti kutoka nyanja na muelekeo tofauti na dunia hii tuliopo yaani kusikia upande wa pili au kwa maneno mengine tunasema dunia ya kiroho iliyopo na huwa ni uwezo wa kusikia sauti za roho takatifu yaani roho zilizojikita katika utukufu wa kumtukuza Mungu na Masters ambao wanachomoza kutoa taarifa kutoka ulimwengu wa roho.

Clairaudience pia inajumuisha maono,muongozo na hekima kutoka katika utakaso wa roho yako mwenyewe na kuwa na uwezo wa kuwa sahihi katika kusikia ushauri wa roho na maono yake.

Katika dunia ya leo nguvu hii watu wengi utawakuta ni wenye kujisifu wanayo na kila mtu utakuta anajitahidi kuiendeleza hata kama sio majaliwa yake na kuanza kutumia njia tofauti tofauti zisizofaa katika kuiamsha na kukuta anakuwa laghai na mtumwa wa shetani au mashetani.

Clairaudience ni moja kati ya nguvu kubwa sana za miujiza ambayo mtu yoyote anaweza kutamani kuwa nayo…
maana huweza kumnufaisha mtu aliyonayo na watu wanaokuzunguka maana katika faida zake ni kuweza kujua yajayo na watu wengi huwa na tamaa ya kuweza kujua mambo kabla hayajatokea.

Kwa maneno mengine,
watu ambao wameikomaza nguvu hii ya miujiza ni watu wenye uwezo mkubwa wa kusikia na kupokea jumbe mbali mbali kutoka katika ulimwengu wa kiroho ikiwa ni kutoka kwa malaika,majini,wanyama,roho za watu waliokufa au hata kupokea ushauri wa Mungu kupitia malaika wake.
na hii kwa watu wengi wasio na maana wala hekima kwao ni simulizi na mambo ya kusadikika kwa maana ni kitu hawajawahi kusikia wala kuona na hata sehemu wanazokuwa wameona ni kwenye Movies na Misalsal yaani Series tofauti tofauti hivyo wanakuwa wanaamini kuwa hakuna kitu kama hicho.
hao ni wale ambao hawana tofauti na wale ambao hawakuamini mifano na watu waliopita kabla yao.

Kuokoa muda na kutofanya maelezo yawe marefu kwanza kabisa tuanze kwa kuangalia ni jinsi gani utajijua kama una nguvu hii ya clairaudience:

Dalili za mtu mwenye clairaudiance ni kama ifuatavyo:

1. Moja utakuwa na tabia ya kuongea peke yako:
Ikiwa ni mtu ambaye unapenda kuzungumza ukiwa peke yako na huwa ni mtu wa kujiuliza maswali na kujijibu mwenyewe pamoja na kujishauri mwenyewe, halafu kujiliwaza mwenyewe basi tambua moja kwa moja una dalili ya kwanza kati ya dalili zinazo muonyesha mtu mwenye kipawa cha Clairaudience.


2. Dalili nyingine ni kama wewe ni mtu wa kujifunza zaidi kwa kupitia kusikiliza kuliko kusoma au kuangalia basi una dalili nyingine ya Clairaudience
Pia kama una tabia ya kushindwa kuwa makini katika kusoma au kujihisi uzito kujibu ujumbe wa maandishi,
kusinzia ukitizama movies au vipindi vya televisheni
na kama ni mtu ambaye unapenda kuhifadhi kitu kwa kutumia kusikiliza kuliko maandishi

kama una tabia ya usikivu na kupenda zaidi kusikiliza kuliko kutumia milango mingine ya fahamu basi unategemewa zaidi kuwa na uwezo wa Clairaudience.

Inaendelea kwenye video

Rakims Spiritual

Show more

 0 Comments sort   Sort By


Up next