JOEL LWAGA - NAFASI NYINGINE (Official Video)
#JOEL LWAGA# NAFASI NYINGINE
Lyrics
(Mmmmh mmmmh mmmmmh)
Mavumbi umenifuta yote
Habari umebadili yooote
Aibu umeondoa yootee
Machozi umenifuta yoteee
Mmmh
Umeniita mwana niliyekuwa mtumwa
Umenisimamisha katika mwingi wa Neema
Na umeniketisha mahali pa juu sana
Ninaucheka wakati uliopita
Nikiufurahia ule ujao
Ninaucheka wakati uliopita nikiufurahia ule ujao
Maana umenipa
Nafasi nyingne (umenipenda tena bila kuchoka)
Nafasi nyingine (Neema yako imeniinua tena)
Nafasi nyingne (Umenipa tena bila kukoma)
Nafasi nyingne Mungu wa Neema
Neema aaaah Mungu wa Neema Neema aaaah aahaaa
Madaktari walisema sitapona tena
Walimu walisema nitafeli
Ndugu na jamaa walisema nimeshindika
Na kumbe wewe waniwazia mema
Umri uliposogea walisema ndoa si fungu langu
Nilipofiwa na mpendwa yule walisema sitaweza tena
Baada tu ya kufilisika sikumwoma wa kuniombea
Na kumbe ndani yao walifurahi niliyopotia
Ninaucheka wakati uliopita
Niliufurahia ule ujao *2
Maana umenipa
Nafasi nyingne (umenipenda tena bila kuchoka)
Nafasi nyingine (Neema yako imeniinua tena)
Nafasi nyingne (Umenipa tena bila kukoma)
Nafasi nyingne Mungu wa Neema
Neema aaaah Mungu wa Neema Neema aaaah aahaaa
(Bwana umenipa)
Nafasi Nyingne
(Kweli umenipa)
Nafasi nyingne
(Mimi nisiyestahili umeniipa)
Nafasi nyingne
Mungu wa Neema (Wa Neema aaaah)
Mungu wa Neema aaaaah
Nafasi Nyingine is a great Gospel and Inspirational Song that means "Another Chance"
its another HIT song from minister JOEL LWAGA who is a multi award winning artist and male artist of the year 2019 EAST AFRICA
Audio Production by : Taz Goemi
Studio : Fishers Records
Video by : Director Ivan