Up next

KUISHI MAISHA MATAKATIFU

1 Views· 06 August 2023
proshabo
proshabo
5 Subscribers
5

#UTAKATIFU

Nini maana ya utakatifu?

Utakatifu unatokana na neno la kiebrania “Qadash” likimaanisha “kujitenga au kutengwa” kwa usafi. Pia kigiriki linatajwa kama “Hagios” likimaanisha kutokuwa na makosa/udhaifu au uchafu.
Hivyo basi utakatifu ni ule usafi kwa kutengwa na Mungu mwenyewe aliye msafi na asiye na makosa/madhaifu.
Tafsiri fupi ya Utakatifu ni usafi wa kiroho na kimwili.

“ kwa kuwa mim ni Bwana, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu…” (Law 11:44-45)
“ kwa maana imeandikwa mtakuwa watakatifu kuwa mimi ni mtakatifu” (1 Pet 1:16)
“watakuwa watakatifu kwa Mungu wao…” Law 21:6-7

Utakatifu si tu kutotenda uovu bali kulazimishwa na Kristo mwenyewe. Mtu asijivunie kwamba hatendi maovu basi yeye ni mtakatifu, la hasha lazima awe anazuiwa kutenda uovu na imani. Huu ndio utakatifu.
#Kweli_muhimu_kuhusu_utakatifu

1.Utakatifu unahusu mwili, nafsi na roho.
Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa, nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wet Yesu Kristo” (1thes 5:23)
Vitu hivi ni kama chenza, chungwa na limao ni matunda jamii moja lakini yenye radha tofauti.
Watu hawawezi kuona nafsi na roho za wenzao bali mwili tu hivyo basi matendo ya mwili yawe safi pasipo lawama.
Utakatifu katika mwili ni pamoja jinsi;

-Unavyokula- mtumishi haifai kula hovyo hovyo na bila ustaarabu
-Unavyoongea-tazama petro alitambuliwa hata kwa kuongea kwake kuwa ni mwanafunzi wa Kristo. Kuna usemi wa mwamini, ni tofauti na mataifa.
-Unavyotembea- pia Petro mwendo wake ulimtambulisha kuwa ni mwanafunzi wa Kristo
Kumbe kuna mwendo pia wa mwamini, si wa kurukaruka au kuyumbayumba kama mlevi bali wa kujiamini kama aliyebeba maono.

-Kuvaa- hapa lazima mavazi yawe ya kujisitiri. Soma 1Tim2:9. Na pia kupangilia vizuri uvaaji. Mpendwa asichanganye uvaaji katika mazingira mbalimbali na apangilie mavazi vizuri kwa unadhifu.

-Pia kuoga, kupasi nguo, na kupaka mafuta na marashi safi.

-mpangilio wa nyumba si kwa kuweka vitu hovyo hovyo pia ni sehemu ya utakatifu
Kuna wakristo hudhania kiroho ni kuishi maishi bila mpangilio (rough) ya hovyo eti tu ili mradi ana uhusiano mzuri na Mungu. Huu ni upotofu kwani watumishi wa Mungu ni watanashati wakubwa: jifunze kwa Yusufu, mfalme Daudi na Sulemani walikuwa nadhifu sana kiasi cha kumvutia kila mtu. Pia vijana Daniel na wenzake walikuwa nadhifu kiasi cha kupendwa na wafalme wa babeli.

2. Utakatifu ni kitu cha kutafutwa
“Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana atakayemwona Bwana asipokuwa nao” (Ebr 12:14)

3. Utakatifu ni lazima kwa anayetaka kumwona Mungu. Rejea Ebr 12:14. Tena Utakatifu ni kuishi na Mungu.

4. Utakatifu ni kujizoeza. Soma Isa 1:16. Tena ni zoezi lisiloisha 1thes 4:7

5. Neno ni takatifu na wanaolifuata lazima wawe watakatifu. Rum 7:12

6. Utakatifu ni makao ya roho mtakatifu. Mdo 2:38 na haiwezekani kuwa mtakatifu pasipo Roho Mtakatifu. Rum 8:28

7.Utakatifu ni upekee; unakuwa maalum ukiwa mtakatifu maana umetengwa na Mungu mwenyewe.

8. Utakatifu ni kuwa nuru. Unakufanya uangaze na uwavutie watu kwa Yesu

9. Utakatifu uhusisha unachotenda na unachowaza. Unachowaza lazima utakitenda.

Jinsi ya kuishi maisha matakatifu

1. Penda kusikia maneno ya Mungu Mithali 4:20

2. Badili mtazamo wako “Jihesabu kwamba umekufa katika dhambi unaishi kwa ajili ya Mungu katika Kristo. Rum 6:11
Mara zote utakutana na majaribu lakini unapaswa kuyaambia nimekufa katika hayo yalikuwa ni sehemu yangu ya maisha ya kale. Mimi ni mpya ka ajili ya Kristo. Akili na mwili vijue hivyo na viishi hivyo.

3. Kutengeneza mahusiano na Mungu. Yaani kujiunga kwa Kristo moja kwa moja kunawezesha utakatifu kuwa maisha rahisi. 1Pet 3:20
Ki ukweli japo twafundisha utakatifu, japo twawashawishi watu kuwa watakatifu lakini daima utakatifu haufundishwi. Kila mmoja wetu anapaswa kuishi maisha matakatifu kwa ajili yake mwenyewe na kwa hiyari. UTAKATIFU HAUFUNDISHWI, KUPEWA AU KULAZIMISHWA.

Utakatifu ni matokeo ya uhusiano na mtu fulani mtakatifu. Kadri tunavyojiweka karibu mtu mtakatifu ndivyo tunavyoweza kuanza kuuishi utakatifu. Ni sawa kabisa na kuweka msumari kwenye mwali wa mshumaa- msumari utapata moto. Msumari hautakuwa na msaada wowote kwa mshumaa bali wenye utapokea joto la mshumaa. Kwa kadri tunavyojiweka karibu na Kristo, ndivyo tunavyozidi kuwa watakatifu. Zab 61:3-4
Mambo yanayokuhusianisha na Mungu ni pamoja na kusikia, kujifunza na kuliishi neno la Mungu na kudumu katika maombi.

4. Kulinda sana moyo wako. Mit 4:23

5. Thamini wokovu kuwa ni wa thamani. Tujifunze kwa Yusufu aligoma kulala na Potifa kwa sababu moja tu aliogopa kumtenda Mungu dhambi pia kuharibu jukumu lake. Nasi tangu tulipookoka tunapaswa kuuona wokovu ni wa thamani kuliko chochote. Mwa 39:8-10 Ebr 2:3

6. Uwe mwepesi kuomba msamaha unapokosea. Kiburi na ubinafsi ni sumu mbaya kabisa ya utakatifu. Makosa yanakushtaki kila unapomkaribia Kristo na hatimaye utakatifu unaondoka kabisa.

7. Jifunze

Show more

 0 Comments sort   Sort By


Up next