Up next

NDOTO NA SIKU ZETU: MAJUMUISHO YA SEMINA: BISHOP GWAJIMA: 16.08.2020

3 Views· 06 August 2023
proshabo
proshabo
5 Subscribers
5

TAREHE: 16.08.2020
Bishop Dr Josephat Gwajima
Somo: Nilipata kutoka Ndoto

MWANADAMU ANA VIPANDE VITATU:
1/ Roho
2/ Mwili
3/ Nafsi

-Mwili wa Mtu unatokana na Mavumbi pumzi ilioingia ndani ya Mtu ndio Roho ya mtu ndio Uhai wa Mtu .Mungu alipo kupulizia Pumzi ndio alipotengeneza Nafsi yako

NAFSI NA VITU VITENDAVYO KAZI NDANI YAKE:
1/ Hisia za mtu
2/ Utashi
3/ Nia
4/ Moyo

-Mtu anapokufa Roho inatoka ndani ya Mwili na nafsi inapotea ndani ya mtu, Kitu chochote kikikuingia kinakaa ndani ya Nasfi na chochote unacho kisikia kinaingia ndani ya nafsi. Shetani akiamua kumfunga Mtu anachagua kwaku mfunga mtu .Mwili wako umetengenezwa na muunganiko wa Baba na Mama yako lakini Roho yako imetoka Mbinguni.

WAISLAMU WANA AINA YA ELIMU MBILI:
1/ ELIMU AHELA (Nyoman )ELIMU DUNIA
2/ ELIMU DUNIA (Faraki)

-Wewe umeshuka kutoka Mbinguni kama ulivyo na hakuna Mtu wa kukuzuia wewe kufanya kitu unachotaka kufanya . Mwili wa Mtu ni combination ya Baba na Mama
Mungu anajivunia Watu Majasiri. Mungu anatembea Duniani kwa kupitia Miguu yako na anapo sema anasema kwa kupitia Midomo yako lakini ukikaa kimya na Mungu ana kaa kimya.

ADUI WA MTU DUNIANI:
1/ Dunia
2/ Mwili
3/ Shetani

-Neno msamaha alipo kuzimu wewe ulivyo na ulivyo umbwa haufanani na Mtu mwingine
-Mfanano Kati ya Eliya na Yohana Mbatizaji, maana Eliya alipo kufa akaja Yohana Mbatizaji kwaumbo la Yohana Mbatizaji lakini ndani Yake alikua na Roho ya Eliya.

VITU WALIVYO FANANA ELIYA NA YOHANA MBATIZAJI:
1/ Wote walikuwa wana kaa Jangwani
2/ Wote walikua wana kula Nzige na Asali
3/ Wote walikua wana Mashuka ya Ngozi
4/ Wote walikua wana Kemea Makuhani na Wafalme

-Unapo zaliwa lazima uwe na kiu ya kufanya kitu fulani lakini kama umezaliwa lakini ukawa hauna kiu ya kufanya kitu chochote basi jua wewe umeibiwa nyota. Ulipo shuka kutoka Mbinguni ulitoka na kitu chakufanya Duniani Shetani apigani na wewe Shetani anapigana na kitu ulicho kibeba ndani yako. Umetoka mbinguni kwakusudi Mungu ana ruhusu upinzani ilikukuwekea ujasili ndani yako Mchawi anao uwezo wakuviona vitu ulivyo vibeba ndani yako. Makaburini kuna Utajili mwingi sana maana Watu Walio lala na vitu walivyo toka navyo Mbinguni ndio maana vita yako haipo Mbali na wewe ila vita yako ipo ndani yako.

-Hatima yako aifunguliwi na mitume pekeake ila Mungu anauwezo wa kuja kufungua hatima yako iliyo fungwa, usilipe ubaya kwa ubaya ila lipa wema kwa ubaya

-Mungu ana luhusu shida ikupate kwa muda Kwajali ya kukunoa kwa Maisha yako ya badae. Kuna mzigo ulio tokanao Mbinguni ili uachie Duniani.

-Maisha yako ayabadilishwi na muonekano ulionao , Kuna mtu anahatima kubwa lakini ameshikiliwa na Mashetani.

Mathayo 1:1-6
“Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu. Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake; Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese; Yese akamzaa mfalme Daudi. Daudi akamzaa Sulemani kwa yule mke wa Uria;”

-Kila Ukoo unakitabu chake Ulipo Fikia Leo sio kwa Mapenzi yako ila ni kwajili ya mapenzi Mungu ndio maana hadi Leo upo. Mtu aliye mwaminifu kwenye mambo Madogo anakuwa mwaminifu hata kwenye mambo makubwa.

Show more

 0 Comments sort   Sort By


Up next