Ni Salama Rohoni Mwangu - Tenzi za rohoni lyrics
#salama #salamarohoni #trending #new #tenzizarohoni #rohoni #tenzi #lyrics #lyricsvideo #gospelmusic #lyricscaptain #gospellyrics #new #trending
Ni Salama Rohoni Mwangu - Dinu Zeno
Tenzi za Rohoni No 23 (It is well with my soul)
Wimbo huu ulitungwa na mwanasheria mmoja mkristo aliyeitwa Horatio Spafford, alitunga wimbo huu kutokana na mambo mazito aliyoyapitia katika maisha yake, Matatizo yake yalianza kwa kufiwa na mtoto wake wa pekee wa kiume aliyekuwa na miaka minne, hiyo ilikuwa ni mwaka 1870
Muda mfupi baadaye (mwaka 1871) moto mkubwa uliozuka huko Chicago Marekani mjini kwake, ukaharibu mali zake nyingi ukizingatia alikuwa ni mwanasheria aliyekuwa amefanikiwa sana. Hilo likafuatana na biashara zake pia kuporomoka kutokana na anguko la uchumi lililotokea mwaka 1873, Hivyo ikambidi apange safari ya kwenda Ulaya pamoja na familia yake, Lakini aliahirisha safari kwa ajili ya kuweka mambo yake ya vibiashara vizuri yaliyokuwa yameathiriwa na moto, hivyo ikambidi msafirishe kwanz mkewe na mabinti zake wanne,akiahidi kuwa atawafuta baadaye.
Lakini Meli ilipokuwa inakatisha bahari ya atlantiki, ilizama ghafla kwa kugongana na meli nyingine na mabinti zake wote wanne wakafariki kwenye ajali hiyo akasalimika mke wake tu, akiwa kule Marekani alipokea ujumbe wa telegrafu kutoka kwa mke wake unaosema “Nimepona peke yangu” ndipo Spafford akaondoka kumfuata mkewe, na huko huko akauandika wimbo huu.