NYIMBO PENDWA ZA KWARESMA 2023. Mtunzi Aloyce Goden KIPANGULA Chang'ombe Catholic Singers Dsm T
Nyimbo Hizi Zote zimetungwa na Mimi Aloyce Goden Kipangula na Kuimbwa na Wanakwaya wakatoliki Parokia ya Chang'ombe Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam ( CHANGOMBE CATHOLIC SINGERS). Ni wajibu wa kila Mbatizwa kuhubiri Injili kwa kadiri ya Karama aliyopewa na Mwenyezi Mungu. Nasi tumekuletea Nyimbo Hizi zenye Tafakari ya kina ili zikufae wewe na Yeyote ambaye utapenda kumshirikisha ili kwa Pamoja kupitia Nyimbo Hizi za Kwaresma Tuweze KUWAPELEKA WATU KWA KRISTO NA PIA KUMLETA KRISTO KWA WATU ( KUTAKATIFUZA MALIMWENGU). NI Nyimbo za Kwaresma lakini pia zinafaa Kuimbwa wakati wowote kwani Katika tungo hizo Hakuna Sehemu hata Moja ambayo nimezungumzia neno Kwaresma Bali nimezungumzia kuhusu umuhimu wa kutubu, kuacha Dhambi, kumgeukia Kristo, kumtegemea Kristo huku Tukiiga mfano wa Mtakatifu Agustino Hippo, Kurudi na kuacha njia ya Dhambi na kufuata njia ya Uzima.