Penina Nyaisare ft Bahati Bukuku Tumughunge (Official Video) 4K Director Banjiman
#GOSPEL #MPYA #+255 762768770
Naitwa Penina Nyaisare, mimi ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Huu ni wimbo wangu wa kwanza kwenye album yangu ya kwanza pia, yenye jina la TUMUGHUNGE: Acha niseme Ahsante kubwa kwa Mungu, lakini pia kwa watu wote walio husika ku support kazi hii hadi kufanikisha kazi hii. Lakini pia nimshukuru Mwimbaji Bahati Bukuku kwa support kubwa aliyoionyesha kwenye kazi hii, pia naishukuru sana B O G Production kwa nguvu walio tia kwenye hii kazi yangu, siwasahau viongozi wa Basata na Cosota kwa ushirikiano mlio uonesha kwakunipokea mimi pamoja na kazi zangu nakunifanya niishi chini ya ulinzi wenu hasa katika sanaa yangu ninayo ifanya. Kijana Banjiman Director wangu wa Because Of God Mungu akuongezee moyo wako wa hekima ulio nao yani kwa vile ulivyo nifanyia mimi uwafanyie na wengine pia.
WaTanzania na wote nawaomba sana mzidi kuniunga mkono nakuniombea kwa sana juu ya kazi yangu ninayoifanya natambua hakuna kazi inayokosa changamoto, kwahiyo nahitaji maombi yenu na faraja zenu juu ya hilo.
NAJUA KUNA MTU ATAKUWA AMEPENDA UBORA WA KAZI HII NA ANATAMANI LABDA APATE HATA NAMBA ZA PRODUCTION ILIYOFANYA KAZI HII, KAMA MTUMISHI WA MUNGU NINAYETAMBUA NINI MAANA YA UPENDO ACHA NIKUSAIDIE NAMBA ZA DIRECTOR BANJIMAN +255 688184191.
Napokea mialiko popote ulipo nitajitahidi nifike wewe nialike tu, nipigie simu namba +255 762768770. Usiache kuniachia Comment yako hapa chini ili nijifunze zaidi, Amina.