Askofu Sylivester Gamanywa - Unyakuo
Kuhusu Mwandishi
Askofu Sylvester Gamanywa (MA - Uongozi na Utawala) ni Mwangalizi Mkuu wa Kitaifa wa mtandao wa makanisa na mashirika ya kitaifa na kimataifa ya WAPO MISSION INTERNATIONAL na ambaye pia ni mwasisi wa vyombo vya habari vya Kikristo vikiwemo Gazeti Msemakweli, WAPO Radio FM na Shalom TV.
Aidha, Askofu Gamanywa kupitia vituo vya Maombezi na Ushauri wa Kibiblia (BCIC) vya jijini Dar Es Salaam na mikoani, amekuwa akiendesha ibada za maombezi kwa maefu ya watu wenye mahitaji binafsi ya kiroho, kiafya na kifamilia ikiwa ni pamoja na kuelimisha jamii katika mambo ya amani na maadili kwa kizazi kipya nchini.
Kuanzia mwaka 2008, amekuwa mwanaharakati wa maadili akiongoza Mpango Mkakati wa miaka 20 (2008-2028) unaolenga kuhamasisha, kuelimisha na kurejesha maadili kwa watu binafsi katika jamii.
Ili kufanikisha maono haya, Askofu anatoa kipaumbele kwa vijana wa kizazi kipya ili kukinusuru na mkengeuko wa maadili. Mojawapo ya mikakati yake ni kuhamasisha vijana kutambua na kuchochea vipaji vyao na kujijenga kwenye maadili ya kiimani kwa Injili ya Kristo.
Kitabu hiki ni sehemu ya mikakati hiyo ambapo ujumbe wake mkuu ni kuwafanya wasomaji wake kuwa tayari kwa ajili ya unyakuo wa kanisa kama maandiko matakatifu yasemavyo
Askofu Gamanywa ameoa mke mmoja anaitwa Happiness na wana watoto wanne ambao ni David, Samael, Excellent na Excel