Azam TV - RC Gambo amcharukia Askofu Kakobe, ataka makanisa yafanyiwe 'audit'
0
0
2 Views·
04 August 2023
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa serikali ina haja ya kutathmini upya uhalali wa baadhi ya madhehebu ya dini ili kuhakikisha eneo hilo linabaki kutekeleza jukumu lake la msingi badala ya kile alichokiita kufanya siasa.
Kauli hiyo inafuatia baada ya Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Zachary Kakobe, kutoa kauli zinazomuhusisha Rais John Magufuli na kumtaka atubu.
Katika mazungumzo yake na vyombo vya habari, Gambo amesema kuwa ni vyema Askofu Zachary Kakobe angejitathmini kabla ya kutoa kauli zinazomuhusu Rais Magufuli.
Show more
0 Comments
sort Sort By