Up next

#HUZUNI KIFO CHA MUME WA JENNIFER MGENDI CHAIBUA SIMANZI UPYA 😭, AONGEA UJUMBE MZITO KWA WAJANE WOTE

1 Views· 15 August 2023
proshabo
proshabo
5 Subscribers
5

#mgendi #jennifermgendi #rip #kifo #gospelmusic

Leo Ni miaka mitatu tangu rafiki yangu, mume wangu Dr Job Chaula apumzishwe na Bwana . Nimeshalia sana, nimeshamlaumu Mungu sana (na kutubu) Ila Kwa kuwa Bwana ananiimarisha nami naona niwaimarishe wengine kidogo kwa haya machache kati ya mengi niliyojifunza mimi binafsi, na niliyojifunza kwa wajane wengine, labda yatamfaa mjane mmoja au mtu mwingine yeyote...

1. NI MSALABA WAKO
Hiki ni kikombe chako ulichopewa kukinywea wewe. Haitawezekana kunywewa na mwingine na kupata uchungu unaoupata. Unayemsimulia au kutaka ashiriki maumivu yako unaweza kumlaumu bure kwa kutojali kumbe si kikombe chake. Hata mjane mwenzio anaweza asihisi maumivu unayosikia kutegemea pia yeye na mwenzi wake waliishije na muda gani umepita tangu afiwe. Kwa hiyo siku zote jitahidi sana ujane wako upambane nao mwenyewe tu na wale ambao Mungu atawagusa wao binafsi. Mwanzoni unatamani uongee na kila mtu labda akufariji nilikuja kugundua wengi unawaboa hasa ambao hawajapitia mtafute mjane mwenzio umsimulie wengine hawakuelewi sana na sio kosa lao.

2. USILAZIMISHE KURUKA HATUA ZA MAOMBOLEZO
Wataalamu wa mambo ya akili wanasema maombolezo ya kufiwa yana hatua 5, Kukataa, hasira, kutafuta mapatano Msongo wa mawazo, kukubali. Acha muda ukuvushe vipindi vyote hivi wengine itawachukua muda mfupi wengine mrefu kutegemeana. Amini tu baada ya muda fulani utaaanza kuwa sawa. Usilazimishe kujisikia ambavyo hujisikii we mwombe tu Mungu akuvushe salama.

3. HUZUNI HAIISHI ILA JIHAHIDI KUIPOTEZEA

Ni kweli maumivu ya mwaka wa kwanza hayalingani na ya mwaka wa pili lakini huzuni haiishi. Ukipita maeneo mliyokuwa mnapita na mwenzako unakumbuka, ukienda kanisani ukitazama alipokuwa anakaa unakumbuka, ukiwatazama watoto unakumbuka unahuzunika, ukiwaona marafiki zake unahuzunika, ukiona njiani matunda aliyokuwa anayapenda unahuzunika, ukiingia chumbani unahuzunika, ukipata hela unahuzunika (angekuwepo tungefurahi wote) ukikosa unahuzunika (angekuwepo angenipa), ukisikia kitu cha kufurahisha angekuwepo ningemwambia, cha kuumiza angekuwepo angenifariji....hakuna muda ambao moyo hutulia.... Ni kipindi kitapita.

4. WATU WAKO WATABADILIKA
Marafiki ambao mlikuwa nao na mumeo kwa namna moja au nyingine hamtakuwa na ukaribu sana kama zamani (hawakuchukii bali ipo hivyo tu). Hata wale marafiki wanandoa 'couples' ambao mlikuwa karibu sana huo ukaribu utakufa au kubaki umeshikiliwa na uzi mwembamba na si kwa ubaya. Unatakiwa kuwa na hekima usilazimishe urafiki maana tayari hamuwezi kuwa watatu kama mlikuwa mnaenda 'outing' pamoja au kutembeleana fahamu haitawezekana tena kuwa tu mwelewa. Ila Mungu atainua watu wengine kabisa wa kuambatana nao na kwa sehemu kubwa watakuwa wajane wenzako, masingle mothers, na wale watu wako ambao kweli ni wako wanakupenda haswa haswa.

5.ZINGATIA AFYA YAKO
Baada ya mwenzako kuondoka, asilimia kubwa hupatwa na magonjwa mbali mbali kutokana na huzuni , kushindwa kula vizuri, kukaa muda mrefu bila kutembea kwani muda mwingi umekaa tu sehemu moja (kipindi cha maombolezo), mashambulizi katika ulimwengu wa roho.

6. HESHIMA KWAKO ITAPUNGUA
Kwa wale waliokuwa wanaheshimiwa sababu ya nafasi za waume zao basi dharau huanza na watu kukupuuza kwa kuwa waliyekuwa wanamheshimu hayupo tena.... Litarajie Hilo na lisikupe shida. Ulikuwa unapokelewa mkoba "Mama Mheshimiwa, Mama Askofu, Mama Mkurugenzi, Shemeji, Madam, Wifi... " unasalimiwa salimiwa hayo yatatoweka taratibu au ghafla kutegemea pia uhusiano uliokuwa nao na watu enzi za uhai wa mzee.

7. WATU KUKUKWEPA
Baadhi ya watu watakukwepa wakiogopa utawaeleza matatizo mbalimbali mara "tumepungukiwa hiki, watoto wamefukuzwa ada, tumeishiwa kodi... nk Mwombe sana Mungu akupe hekima katika hili Mungu akupe uwezo wa kupata kakipato kako hata kadogo. Jitahidi kuanza shughuli za kukuingizia kipato mapema tena jilazimishe tu.

8. KUBALI MATOKEO
Kubali matokeo kuwa yashatokea basi hakuna jinsi ni kukubaliana na hali halisi. Uchumi utabadilika, maisha yatabadilika, nk yakubali kuwa ndiyo mapemzi ya Mungu kwako kwa wakati huo.

9. PUUZA MANENO
Maneno huwa mengi sana kipindi cha mwanzo ya kukatisha tamaa, ukifanya kazi wengine watasema huna uchungu ulitakiwa ukae kwanza kuomboleza, ukikaa uomboleze halafu uanze kuwaomba misaada watasema wewe mvivu unawalemea, utasingiziwa na kuzushiwa, utapendwa na wengine na kuchukiwa na wengine nk. Ni kipindi cha aibu na kuhisi kama watu wanakucheka au kukuzomea ni kipindi tu kitapita.

10.USIKAE PEKE YAKO
Kipindi cha mwanzoni ni kigumu sana jitahidi sana usikae peke yako kwani unakuwa na hofu na huzuni nyingi. Jilazimishe kujichanganya na watu inasaidia sana ingawa ni ngumu unatamani ukae peke yako ulie tu. Kajiunge na kwaya, au anza kuhudhuria vikundi vya kinamama wenzio unapoabudu na kwingineko inasaidia sana.

MUNGU AKUBARIKI SANA

USISAHAU KU SUBSCRIBE

Show more

 0 Comments sort   Sort By


Up next