INJILI NI MOTO/ HEBU TAZAMA USIPO ACHA DHAMBI?(2)
IJUE NJIA YA KUONGEA NA MUNGU NA IJUE NJIA YA KUKUSAIDIA KUMJUA MUNGU NA NENO LAKE..
*1️⃣ NJIA YA KUONGEA NA MUNGU NI MOJA TU MAOMBI, UKIOMBA NA MUNGU ANAKUSEMESHA* imeandikwa hivi👇
*👉Yeremia 33:3 Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.*
👆🏻Usipoita hakuna siku Mungu ataitikia..
✔Inawezekana bado haujanielewa, ni hivi usipohoji hakuna siku Mungu atahojiana na wewe..
*👉Isaya 43:26 Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.*
✔Kwahiyo ukitaka Mungu aseme hakikisha na wewe unasema (OMBA), ukitaka uhojiane na Mungu hakikisha unalo jambo la kumhoji Mungu vinginevyo hakuna siku utamsikia Mungu akisema na wewe 👈hili ni jambo mhimu sana kama unataka kuwa na mahusiano ya karibu na Mungu yanayokupa kumsikia MUNGU pindi anaposema na wewe..
2️⃣Njia za kukusaidia ili ulijue neno la Mungu..
*NENO LA MUNGU UTALIJUA IKIWA UTAWEKA MIKAKATI INAYOELEWEKA*
(i) Mikakati ya kusoma biblia yako, kama hauna mda wa kusoma biblia hakuna siku utalijua neno la Mungu
(ii.) Mikakati ya kupenda kuhudhuria vipindi vya ibada kanisani kwenu,
*▶️ Ni hivi kanisani ndipo tunapopata mafundisho ya neno la Mungu, lakini pia ndipo tunapobadilishana mawazo na udhoefu juu ya Mungu, kwahiyo kama wewe si mtu wa ibada hakuna siku utalijua neno la Mungu..*
(iii) Mikakati ya kupenda kujifunza na kusikiliza mafundisho mbalimbali ya neno la Mungu..
*▶️Mara ngapi unapata mda wa kusikiliza vipindi vya neno la Mungu redioni au katika runinga yako? Mara ngapi unapenda kufuatilia vitu vyenye tija na maisha yako kwenye mitandao ya kijamii hususa ni mafundisho ya neno la Mungu? Mara ngapi unanunua vijitabu vya mafundisho ya neno la Mungu? 👈ni hivi usipojipa wigo mpana wa kufuatilia neno la Mungu hakuna siku utalijua neno la Mungu..*
(iv.) Kupenda kuuliza maswali ya Kibiblia kwa watumishi wa Mungu..
▶️Takwimu za kibiblia zinaonyesha yakwamba katika wale mitume kumi na wawili wa Yesu walioonekana kulijua neno vizuri kuliko mitume wengine ni wale waliopenda kumwuliza Yesu sana maswali, moja kati ya hao ni PETRO, YAKOBO na YOHANA..
Mfano👇
⛔Maswali ya PETRO
*◾Mathayo 15:15 Basi Petro akajibu, akamwambia, Tueleze mfano huo.*
*◾Mathayo 18:21 Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?*
*◾Mathayo 19:27 Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?*
⛔Maswali ya YAKOBO na YOHANA
*◾Marko 13:3 Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, kuelekea hekalu Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea walimwuliza kwa faragha,*
*◾LUKA 9:54 Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?*
👆🏻Nimekupitisha kwenye hii mifano michache ili uone yakwamba PETRO, YAKOBO na YOHANA ni mitume pekee wa Yesu waliolijua neno la Mungu kuliko mitume wengine kwasababu ni watu waliopenda kumwuliza Yesu maswali ili kujifunza, ndiyo maana kwasababu ya ufahamu wao mkubwa juu ya neno la Mungu katika biblia hawa ndiyo mitume pekee wa Yesu walioandika nyaraka 👈hakuna mtume mwingine aliyeandika waraka katika wale mitume kumi na wawili wa Yesu zaidi ya PETRO, YOHANA na YAKOBO..
*✔Nachotaka kukufundisha nikuwa kama unataka kumjua Mungu na neno lake jifunze kuwa mtu wa maswali, Jifunze kumwuliza Roho mtakatifu aliye mwalimu mkuu lakini pia jifunze kuwauliza watumishi wa Mungu maswali mbalimbali ya kibiblia, UDADISI WAKO WA MAMBO UTAKUFANYA ULIJUE NENO LA MUNGU KWA UPANA WAKE NA UMJUE PIA MUNGU WAKO VIZURI..*
🔶Mwisho..
*👉Waefeso 1:17 Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;*
*JIFUNZE ZAIDI HAPA*
👇👇👇👇👇
https://youtu.be/pc5yysyDe3c
*SHARE UJUMBE HUU KWA WENGINE NA MUNGU WA MBINGUNI AKUBARIKI SANA*
*TUZISIKILIZE NA KUZIFUATA AMRI ZA BWANA MAANA YEYE NDIYE ATUFUNDISHAYE NA KUTUONGOZA ILI TUPATE FAIDA*
Bwana Yesu Asifiwe.
Wapendwa katika Bwana nimetafakari sana upendo wa Mungu ndani ya maisha ya mwanadamu nikagundua ni mkuu mno tena sana jamani.
Lengo la Mungu wetu ni sisi kukaa na yeye tu siku zote, hapendi tupotee kabisa. Maana mpango wa Mungu ni sisi kuishi naye milele. Ndio maana alipoona mwanadamu wa kwanza ameharibu alimtoa mwanawe pekee afe msalabani ili atuokoe kutoka vifungoni na turejee kwake.
Mungu ndiye aliyetuumba, hivyo kwa vyovyote vile anatujua kuliko sisi tujijuavyo yaani baba zetu wa kimwili wanatufahamu sana kwasababu wao ndio waliotuzaa pia.
Anaposema Mimi ndiye nikufundishaye na kukuongoza ktk njia inayopasa ili upate faida ni kweli kabisa, kwani pasipo kuongozwa naye sisi ni wa kupotea tu, kwasababu mwanadamu pasipo Mungu si kitu. Katika Mungu Yesu Kristo tunaishi, tunakwenda na kuwa na uhai wetu.