MITIMINGI # 761 TENDO LA NDOA KWA WANANDOA NDIO LINALOBORESHA NDOA YAKO
VICHOCHEO VINAVYOCHANGIA USALITI KATIKA NDOA
Miongoni mwa wanandoa wanafikiri kuwa kufanya tendo la ndoa mara chache ndio inaongeza uimara wa ndoa! No Msingi na uimara wa ndoa unapimwa kupitia TENDO LA NDOA.
Tendo la ndoa ni Kipimo cha mahusiano yako na upendo baina ya wanandoa; wanandoa walio wengi wakati mahusiano yao ni mapya hufanya tendo la ndoa mara kwa mara.
Kama wanandoa hawajafanya Tendo la ndoa kwa muda wa mwezi mmoja, ni alama ya wazi kuwa Hawaelewani, ndoa yao imeingia misukosuko.
Utafiti wa kisaikolojia unaonesha kwamba ili akili ya mwanaume ikae sawa anahitaji kula tendo la ndoa lililo na utoshelevu.
NB: KUFANYA RENDO LA NDOA MARA KWA MARA NI ULINZI MKUBWA SANA HASA KWA MWANAUME
Mch na Mwl. Dr. MITIMINGI p. Senior Pastor #WCC & Counseling Psychologist #BLCCC +255 713 18 39 39