TAFUTA NJIA YA UTAKATIFU (2)
Milele ni muda mrefu sana sana sana sana.
Sasa huo muda mrefu sana sana sana sana uwe bila Kristo, ukiwa umetengwa na Mungu katika ziwa liwakalo kwa moto na kiberiti ambao funza wake hawafi na watu husaga meno usiku na mchana utakuwa ni muda mrefu mno mno mno wa mateso makali na vilio.
Mungu aliupenda mno ulimwengu akamtoa Mwanae wa pekee Yesu Kristo ili aje afe msalabani kwa ajili yako na yangu ili alipe gharama kwa ajili ya dhambi zako na zangu.
Maandiko yanasema kuwa alijeruhiwa kwa ajili ya makosa yako na yangu, alichubuliwa kwa ajili ya maovu yako na yangu, adhabu ya amani yetu iliwekwa juu Yake na kwa kupigwa Kwake sisi sote tumepona.
Maandiko tena yanasema kuwa kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanae wa pekee ili kila ameaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.(Yohana 3:16)
Usipomwamini Mwana pekee wa Mungu utapotea milele.
Utakufa na kuingia kwenye umilele bila Mungu.
Yesu alisema kuwa Yeye Ndiye njia, kweli na uzima na hakuna mtu ajaye kwa Baba isipokuwa kwa njia Yake Yeye.
Hakuna njia nyingine ya kumwendea Mungu isipokuwa kwa njia ya Yesu Kristo, kumwamini ili aziondoe dhambi zako na uweze kuishi maisha ya ushindi juu ya dhambi maana kila mmoja wetu anahitaji kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao mtu asipokuwa nao hawezi kumwona Mungu.
Maandiko yanatuambia kuwa hakuna Jina jingine ambalo tumepewa wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo ila Jina la Yesu.(Matendo 4:12)
Hakuna dini inaweza kutuokoa maana hakuna dini iliyokufa kwa ajili ya dhambi zetu.
Dini haiwezi kumfikisha mtu kwa Mungu maana dini sio Njia ya kwenda kwa Baba.
Yesu Ndiye njia ya kwenda kwa Baba.
Maandiko yanatuambia kuwa uzima wa milele ndiyo huu, kumjua Mungu wa kweli wa pekee na Yesu Kristo aliyemtuma.
Yesu pekee Ndiye awezaye kumfunua Baba kwetu.
Mtu wa Mungu kwanini upotee.
Mwamini Yesu leo.
Fungua mlango wa moyo wako na maisha yako Yesu aingie ndani akusamehe na kukuokoa na dhambi zako.
Unahitaji kuzaliwa mara ya pili maana mtu asipozaliwa mara ya pili hataweza kuingia katika Ufalme wa Mungu wala wa mbinguni.
Geuka leo uiache dunia na mambo yake uje kwa Yesu akuokoe na kukusafisha na dhambi zako.
Yesu alisema "Njooni kwangu nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha." (Mathayo 11:28)
Hakuna pumziko lolote nje ya Yesu.
Dhambi ina nguvu mno juu ya mtu anapokuwa nje ya Yesu.
Dhambi inasumbua na kulemea mtu akiwa nje ya Yesu.
Wakati Yesu anakaribia kuzaliwa, malaika alizungumza na baba yake Yesu wa kufikia na kumwambia kuwa mkewe atazaa mtoto Mwanamume na Jina Lake atamwiita Yesu maana Yeye Ndiye atakayewaokoa watu Wake na dhambi zao. (Mathayo 1:21)
Bila Yesu huwezi kuokoka na dhambi zako.
Dhambi zitakuangamiza na kukupoteza.
Maandiko yanamnukuu Yesu akisema tutwae nira Yake tujifunze Kwake maana Yeye ni mpole na mnyenyekevu wa moyo nasi tutapata raha nafsini mwetu.
Bila Yesu huwezi kuwa na raha nafsini mwako.
Raha nafsini na maishani inakuja kwa kumpata Yesu na kuishi sawasawa na mafundisho Yake na Neno Lake.
Mtu wa thamani wa Mungu kwanini upotee na kuangamia wakati Yesu alishakuja ili usipotee wala usiangamie?
Yesu Mwenyewe alisema kuwa amekuja kutafuta na kuokoa kilichopotea.
Mtu wa thamani wa Mungu kila mmoja wetu bila Yesu atapotea na kuangamia.
Ni ndani ya Yesu na Yesu pekee ndipo tunapopatikana na kuokolewa.
Mtu wa Mungu wa thamani mbinguni ni halisi sana na pia jehanum ni halisi mno.
Mbinguni ni mahali pa raha, amani na furaha ya milele.
Jehanum ni mahali pa maumivu, mateso, kilio na kusaga meno milele.
Bila Yesu unakoelekea ni jehanum.
Jehanum ni mahali pa mateso, maumivu, kilio, kusaga meno milele.
Maandiko yanasema mtu mwenye busara huiona hatari inakuja akajificha lakini wapumbavu huendele mbele na huangamia.
Pa kujificha na hatari inayokuja ni kwa Yesu.
Mtu wa thamani wa Mungu, njoo kwa Yesu ujifiche na hatari inayokuja.
Ukichagua kumpuuza Yesu basi jua kuwa unaelekea kwenye hatari ya umilele bila Mungu.
Maandiko yanasema mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke lazima tu atakufa.
Na wanadamu wameandikiwa kufa mara moja na baada ya kifo ni hukumu.
Hakuna kiasi cha maombi ambayo utaombewa ukishakufa ambacho kinaweza kukusaidia.
Maana hata kabla watu hawajagundua kuwa umekufa utakuwa umesha hukumiwa.
Na hukumu ya Mungu haina rufaa.
Yesu pekee Ndiye awezaye kukuepusha na hukumu ijayo.
Maandiko yanasema "Heri wafu wafao katika Bwana kuanzia sasa, wapate kupumzika baada ya taabu zao na matendo yao yafuatana nao."
Usipokufa katika Bwana haitakuwa heri kwako.
Usipokufa katika Bwana hautapumzika.
Haijalishi wangapi wanaitakia roho yako ipumzike mahali pema peponi.
Roho hazipumzishwi mahali pema peponi kwa kuombewa bali kwa maamuzi ya kumkubali Yesu tungali hai mtu wa thamani wa Mungu.
Ukimtaa Yesu leo mbele za watu Yeye Naye atakukataa mbele za Baba Yake.
Mtu wa thamani wa Mungu njoo kwa Yesu leo.
Mpe maisha yako.
Zaliwa mara ya pili.
Okoka.