MADHARA YA DHAMBI YA UZINZI - PASTOR BARAKA BUTOKA
Katika Kitabu cha WAEFESO 5:3 imeandikwa “Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;”. Mtume Paulo anatuasa kuwa kwa watakatifu neno la uasherati au uchafu lisitajwe kamwe. Neno uasherati au uzinzi kwa mara nyingi hutumika kumaanisha jambo moja. Uasherati ni pale tendo la ndoa likifanywa na mtu kabla hajaoa au kuolewa. Uzinzi kwa upande mwingine, ni tendo la ndoa likifanywa na mmojawapo wa wanandoa pamoja na mwanaume/au mwanamke asiyehusika katika hiyo ndoa. Hata hivyo Biblia inasema kila dhambi ina mshahara wake ambao ni mauti.
More updates:
* Blog: https://www.gospomedia.com
* Gospo Media App - http://bit.ly/2p6Hjkm
* Facebook: http://bit.ly/2yUN1aL
* Instagram: http://bit.ly/33uYSdN