Up next

ORCHESTRA MKWAWA - WIKIENDI IRINGA MPIGA TUMBA KAKOBE

2 Views· 04 August 2023
proshabo
proshabo
5 Subscribers
5

BENDI ZA SHULE ZA SEKONDARI
Mkwawa Jazz Band katika mtindo wao wa Ligija.Bendi hii ilikuwa moja ya bendi mbili za wanafunzi waliokuwa wakisoma Mkwawa High School kati ya mwaka 1969 na 1971. Kila Jumapili mchana bendi hizi mbili ziliporomosha muziki katika mfumo uliojulikana kama bugi, katika ukumbi wa Community Center pale Iringa. Bugi lilikuwa dansi lililoruhusu wanafunzi na watoto wadogo kufaidi dansi. Dansi lilianza saa nane mchana na kibali cha bugi kiliisha saa kumi na mbili kamili, pombe zilikuwa marufuku wakati wa bugi. Katika miaka hiyo shule za sekondari nyingi zilikuwa na bendi na bendi hizi nyingine zilikuja kuwa maarufu na hata kuja kutoa wanamuziki maarufu sana. Na kwa kuwa kulikuwa na utaratibu mzuri wanafunzi wengi waliokuwa wanamuziki wakati huo walikuja kuendelea na kuwa watu muhimu katika nyanja mbalimbali kitaifa. Kwa mfano katika bendi hiyo ya Mkwawa iliyoimba na hata baadae kurekodi wimbo wangu wa leo, wanamuziki wake wote walikuja kuwa watu wenye nafasi muhimu Kitaifa. Mpiga solo Sewando alikuja kuwa mwalimu wa ‘electronics’ chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na pia ndie alikuja kuwa mwanzilishi wa bendi ya TZ Brothers. Sewando ambaye mwanae sasa ni producer maarufu wa muziki wa ‘kizazi kipya’, alianza muziki akiwa Kwiro Secondary ambako nako kulikuwa na bendi iliyowahi kurekodi nyimbo maarufu wakati huo, na hata kuwa chanzo cha baadhi ya mitindo iliyotumiwa na Morogoro Jazz band. Sewando alianza kupenda electronics wakati huo, na kuwa fundi wa vyombo vya bendi yake ya shule kiasi cha kupata jina la ‘The Mad Scientist’. Masanja alikuwa mpiga rhythm wakati huo na hatimae alikuja kuwa rubani wa ndege. John Mkama aliyepiga bezi alikuja kuwa mwandishi wa habari mahiri. Manji aliyepiga rhythm pia alikuja kuwa mhandisi wa ndege, na miaka mchache iliyopita alianzisha bendi iliyoitwa Chikoike Sound, na kwa sasa ana shule nzuri ya muziki Tabata, Dar es Salaam wakati muimbaji Danford Mpumilwa ni mwandishi maarufu, nae pia ndie alikuwa mwanzilishi wa bendi ya Serengeti ya Arusha. Mpiga tumba katika wimbo huo ni kiongozi maarufu wa dini mwenye wadhifa wa Askofu Mkuu. Hivyo kushiriki katika muziki hakukuwafanya wanamuziki hawa waishie kuwa wahuni au walevi walioharibikiwa kimaisha au kushindwa kuendelea ma masomo. Bendi ya pili ya Mkwawa Secondary ilikuwa ikipiga muziki wa kizungu na hasa wa mtindo wa soul. Bendi hii iliitwa ‘The Midnight Movers’ ikiwa na wanamuziki kama Kafumba, Martin Mhando. Hans Poppe, Deo Ishengoma, amboa waliohai ni watu wenye nyadhifa muhimu katika jamii. Kuwa mwanamuziki hakukuwa tiketi ya kuwa muhuni. Kama nilivyosema shule nyingi za sekondari zilikuwa na bendi, pale Dodoma Secondary kulikuwa na bendi kiongozi wa bendi hii alikuwa Patrick Balisidya aliyekuja kuwa mwanamuziki maarufu alipokuja kuanzisha Afro 70.

Show more

 0 Comments sort   Sort By


Up next